Yanga Yatolewa Kombe La Mapinduzi na Simba Kwa Penati ya 4-2 ............Sasa ni Simba vs Azam fainali Mapinduzi Cup2017
Yanga
imeendelea kusulubiwa kwenye mashindano ya Mapinduzi Cup baada ya
kujikuta ikichezea kichapo kutoka kwa Simba kwenye mchezo wa nusu
fainali ya pili kwa mikwaju ya penati 4-2 kufatia dakika 90 kumalizika
bila timu hizo kufungana.
Baada
kichapo cha 4-0 kutoka kwa Azam FC, Yanga imeondoshwa kwenye michuano
hiyo na kuziacha Simba na Azam zikutane kwenye mchezo wa fainali ambao
utachezwa siku ya Ijumaa January 13, 2017 ikiwa ni siku moja baada ya
kilele cha Mapinduzi ya Zanzibar.
Golikipa
wa Simba Daniel Agyei ndio alikuwa shujaa kwa upande wa Simba hususan
kwenye changamoto ya mikwaju ya penati. Agyei ameokoa penati mbili za
Deogratius Munishi na Mwinyi Haji huku yeye akifunga penati yake baada
ya Mkude kufunga ya kwanza.
Wachezaji wa Simba waliofunga penati: Jonas Mkude, Daniel Agyei, Mzamiru Yassin na Javier Boukungu
Method Manjale ni mchezaji pekee wa Simba aliyekosa penati ambayo iliokolewa na golikipa wa Yanga Deogratius Munishi.
Simon
Msuva na Thaban Kamusoko ndio wachezaji pekee wa Yanga waliofunga
penati zao huku Deogratius Minish ‘Dida’ na Mwinyi Haji penati zao
zilitua kwenye mikono ya golikipa wa Simba Daniel Agyei.
No comments