Header Ads

Happy Birthday Tanzania...



Happy Birthday Tanzania...



Tanganyika ni jina la kihistoria la sehemu kubwa ya Tanzania ya leo, yaani ile yote isiyo chini ya serikali ya Zanzibar.
Kwa sababu za kisiasa, mara nyingi huitwa "Tanzania bara" ingawa ina visiwa pia, hasa Mafia na Kilwa.
Tanganyika ilikuwa eneo lindwa la Uingereza kuanzia 1919 na nchi huru kati ya 1961 hadi 1964, mwaka wa kwanza kama ufalme, halafu kama jamhuri.
Mwaka 1964 iliungana na Zanzibar na kuwa sehemu ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.


Chanzo katika koloni la Kijerumani

Maeneo yaliyoitwa baadaye (1920) "Tanganyika" yaliunganishwa mara ya kwanza tangu mwaka 1886 kama koloni la Ujerumanilililoitwa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Kabla ya kufika kwa ukoloni kulikuwa na madola madogo mbalimbali na maeneo madogo ya kikabila.
Kanda la pwani pamoja na njia za misafara kuelekea Ziwa Tanganyika vilikuwa chini ya athira ya Usultani wa Zanzibar.
Tangu mwaka 1885 Karl Peters, kwa niaba ya Shirika la Ukoloni wa Kijerumani (Gesellschaft für Deutsche Kolonisation) alianza kufanya mikataba na watawala wenyeji katika maeneo ya UsagaraNguruUseguha na Ukami iliyoweka msingi wa madai yake ya kuchukua utawala mkuu wa maeneo hayo.
Uenezeaji wa Wajerumani uliendelea hasa baada ya kushinda upinzani katika vita ya Abushiri na vita dhidi ya Wahehe.
Koloni lile la Kijerumani lilikuwa kubwa kuliko Tanganyika ya baadaye, maana ilijumlisha pia maeneo ya Rwanda na Burundi pamoja na sehemu ndogo ya Msumbiji.
Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia (1914 - 1918) koloni hilo la Kijerumani lilitekwa na majeshi ya Uingereza na Ubelgiji.
Mkataba wa Versailles wa mwaka 1919 ulikuwa na kanuni za kuchukua makoloni yote ya Ujerumani na kuzikabidhi kwa mataifa washindi wa vita. Sehemu kubwa ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani iliwekwa chini ya utawala wa Uingereza, kasoro maeneo ya Rwanda na Burundi yaliyokabidhiwa mikononi mwa Ubelgiji.

Tanganyika Territory ya Kiingereza baada ya kuondoka kwa Wajerumani

Bendera ya koloni ya Tanganyika.

Mwaka 1919 sehemu kubwa ya koloni la Kijerumani ilikabidhiwa rasmi mikononi mwa Uingereza kama eneo la kudhaminiwa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa kulingana na kifungo 22 cha mkataba wa Versailles.
Mwaka 1922 Shirikisho la Mataifa lilithibitisha hatua hiyo na kuamua masharti ya kukabidhi.
Waingereza walihitaji jina jipya kwa ajili ya koloni hilo na tangu Januari 1920 wakaamua kuliita "Tanganyika Territory" kwa kutumia jina la ziwa kubwa upande wa mashariki ya eneo. 

Uhuru na Muungano na Zanzibar

Tanganyika ilipata uhuru wake tarehe 9 Desemba 1961 
Mwaka 1964 imeunganika na Zanzibar kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Leo hii neno "Tanganyika" latumiwa wakati mwingine kutaja sehemu ya Tanzania isiyo Zanzibar, hasa na watu ambao hawapendi muundo wa serikali mbili tu (ile kuu na ile ya Zanzibar) ndani ya muungano na wanadai kuwa na serikali ya tatu, yaani ile ya Tanganyika.

No comments

Powered by Blogger.