Header Ads

NISHA: Mimba Hii Ingekuwa ya Baraka The Prince Inge.........

Nyota wa filamu nchini ambaye siku za karibuni amekuwa akihaha na ujauzito alionaonao bila kumuweka wazi muhusika, amekanusha kuwa ujauzito huo ni wa msanii Baraka The Prince.

Nisha Baby amefunguka kuhusiana na hilo akiwa katika kipindi cha FNL cha EATV, na kusema kuwa endapo ujauzito huo ungekuwa wa Baraka kama inavyosemwa na wengi basi ungetoka wenyewe mapema sana kwa kuwa Baraka ni miongoni mwa wanaume asiowapenda kabisa duniani.

"Kama hii mimba ingekuwa ya Baraka, ingetoka yenyewe, wala isingesubiri" Alisema Nisha.
Kuhusu muhusika wa ujauzito huo, Nisha ameendelea kufanya siri na kuapa kutomtaja kabisa hata siku moja licha ya watu kutaja baadhi ya majina ya watu maarufu ambao amekanusha kuwa siyo wahusika.

Katika hatua nyingine Nisha aliweka wazi kuwa anatarajia kujifungua mtoto wa kiume, licha ya kuwa bado hajamtafutia jina.

Kuhusu mazingira aliyopata ujauzito huo, Nisha ambaye alijikuta akimwaka chozi studio, alisema mwanaume aliyempa ujauzito alimlazimisha kufanya naye mapenzi, na kwamba ahaikuwa ridhaa yake na ndipo ikatokea hivyo.

Kuhusu hoja za baadhi ya mashabiki kuwa ni kwanini hakuitoa kama hakuwa tayari, Nisha alisema imani yake ya dini haimruhusu kutoa mimba.
"Ingawa kuzidi ni dhambi, lakini kutoa mimba pia ni dhambi na dini zote haziruhusu kutoa mimba"

No comments

Powered by Blogger.