Aliyetuhumiwa Kumpatia Kiwanja ‘Feki’ RC Makonda, Aeleza Uhalali wa Umiliki wa Eneo Hilo
Baada ya waziri wa ardhi William Lukuvi kudai eneo la ekari 1500 alilopewa RC Paul Makonda kwaajili ya ujenzi viwanda vidogo vidogo kuwa ni eneo la serikali, mmiliki wa eneo hilo mfanyabiashara Mohamed Iqbal ametoa vielelezo vya umiliki wa eneo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Ijumaa hii Kamugisha Katabara ambaye ni mwakilishi wa Mohamed Iqbar katika ukumbi ya jengo la Red Cross jijini Dar es salaam amesema:
Kufuatia taarifa iliyotolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi mnamo tarehe 27, Februari mwaka huu ya kuwa ndugu Mohamed Iqbar alisema kuwa lile sio eneo lake ni mali ya serikali amemdanganya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa kumpatia eneo la ardhi lililopo Lingato Kisarawe 11, Kigamboni Dar ambalo si mali yake bali ni mali ya serikali, kufuatia kushindwa kesi kati yake na wananchi.”
Aliongeza, “Kufuatia tuhuma hizo imewasikitisha wataalamu wanaotambua jambo hilo kumuondolea heshima ndugu Iqbal ndipo walipoita waandishi hao kufikisha ukweli kwa umma juu ya mambo haya matatu ikiwa ni pamoja na umiliki wa eneo, utaratibu wa kukabidhi eneo kwa mkuu wa mkoa huyo, na hukumu ya kesi aliyoizungumzia mhe Waziri wa ardhi. Ndugu Iqbal ni mmiliki halali wa eneo la ardhi lenye ukubwa wa ekari 3500 lililopo eneo tajwa hapo juu. Eneo hilo alinunua tangu mwaka 2005 kutoka kwa wananchi wa eneo hilo ambao waliuza kwa hiari yao wenyewe bila kushurutishwa na kwa kufuata taratibu zote za kisheria za ununuzi wa ardhi.”
Aidha Katabara alitoa uhalali wa umiliki wa eneo hilo huku akisema kuwa endapo zitahitajika zitawekwa bayana nakala pamoja na picha.
“Ushahidi wa nakala za barua za mawasiliano kati ya ofisi ya serikali ya mtaa wa Lingato,muhtasari ya vikao vya maamuzi ya serikali za mitaa na mikutano na wananchi waliomiliki maeneo hayo ipo. Aidha nakala za risiti zipo na malipo ya ushuru wa serikali kama sheria inavyotaka na mikataba ya mauziano ya maeneo ya ardhi na picha za wamiliki wa maeneo wakipokea fedha za malipo na mauziano ya ardhi zipo na zitawekwa bayana pale zitakapohitajika.”
No comments