MFAHAMU RAISI MASIKINI ZAIDI DUNIANI ANAYEISHI KIJIJINI
Ni
kawaida kukuta maisha wanayoishi Wanasiasa ni tofauti na wapiga kura
wao lakini sio hivyo kwa Rais wa Uruguay ambae anaishi kwenye maeneo ya
mashambani na anatoa sehemu kubwa ya kipato chake kusaidia watu
masikini.
1. Yani nguo zake zinafuliwa kawaida na kuanikwa nje tu, pia maji anayotumia ni ya kisima ambacho kina magugu mengi.
2.
Analindwa na Polisi wawili na mbwa na aliikataa kukaa kwenye nyumba ya
serikali aliyopewa na badala yake kaenda kuishi kwenye nyumba ya mke
wake huko mashambani ambako kuna mazingira ya kimasikini sana ikiwemo
barabara mbovu nje kidogo ya mji wa Montevideo.
3. Rais na mkewe hufanya kazi ya kuotesha maua wao wenyewe yakiwa ni maisha ya kipekee kusikia ni ya Rais wa nchi.
4. Mujica anatoa asilimia tisini 90% ya mshahara wake wa kila mwezi kusaidia watu masikini huku akisema ‘naweza kuonekana kama mzee wa jadi lakini maisha haya nimeyachagua mwenyewe, naweza kuishi vizuri na kile nilichonacho.
5.
Rais huyu kwa mwezi matumizi yake hayazidi shilingi milioni moja laki
nne za Kitanzania ambapo kwenye kuorodhesha kiwango cha kipato cha kila
kiongozi kwa mwaka na mali binafsi ikiwa ni lazima nchini humo kwa
viongozi mbalimbali wa serikali mwaka 2010, alikutwa na kiasi cha dollar
$ 1,800 tu kiasi ambacho hakizidi shilingi milioni tatu za kitanzania.
6. Gari anayotumia ndio hiyo picha ya kwanza hapo juu ambayo ni ya mwaka 1987 aina ya Volkswagen Beetle.
7.
Mujica aliwahi kupigwa risasi mara sita na alitumikia kifungo miaka 14
jela ambapo muda wake mwingi kizuizini alikua katika mazingira magumu na
kutengwa, mpaka alipoachiliwa huru mwaka 1985 wakati Uruguay ilivyorudi
kwenye demokrasia.
8. Akiwa jela Mujica anasema hali ile ilimbadilishia mtazamo wake juu ya maisha na anakwambia ‘mimi naitwa rais maskini lakini mimi wala sihisi umaskini
wowote, watu masikini ni wale ambao kazi yao ni kuishi maisha ya
gharama ambayo inawasababisha kufanya kazi sana ili waendelee na maisha
ya gahrama na kupata zaidi’
- Mujica aliwalaumu viongozi wengi wa dunia ya kuwa na “upofu wa kutaka kukua na matumizi, kiasi kwamba isipokua hivyo itakuwa mwisho wa dunia.
No comments