Nuh Mziwanda Akana Kutoka na Shilole Jijini Mwanza
Msanii
Nuh Mziwanda ambaye bado anafanya vyema na wimbo wake 'Jike shupa'
amekanusha tetesi za yeye kuwa pamoja na mpenzi wake wa zamani Shilole
jijini Mwanza siku mbili hizi.
Akiongea
kwenye kipindi cha Planet Bongo, Nuh Mziwanda anasema ni kweli alimuona
Shilole Mwanza kwenye club ambayo yeye alikuwa anafanya show na
aliambiwa kuwa yupo pale lakini hakukutana naye wala ku-kiss na yeye
kama ambavyo watu wanadai kuwa waliwaona wakali hao wakiwa pamoja na
waki kiss.
"Mimi
nimekuja Mwanza kwenye show zangu nimekutana naye tu Club hivyo mimi
siwezi kumkataza mtu kuingia sehemu hivyo hilo ni jambo la kawaida, mimi
mwenyewe niliambiwa yupo humu so sikujali maana mimi nilienda kufanya
kazi na yeye alikwenda kufanya kazi kimpango wake. Kwa hiyo hayo maneno
mengine yanayoongeleka mimi mwenyewe siyajui mimi nimekuja Mwanza
kutafuta pesa" alisema Nuh Mziwanda
Mbali
na hilo Nuh Mziwanda anasema kwa yeye saizi ni mume wa mtu hivyo hawezi
kufanya mambo ya ajabu ajabu kama hayo kwa kuwa yeye anajiheshimu na
kuheshimu ndoa yake
"Mimi
nimeoa najiheshimu siwezi kufanya vitu ambavyo si vya maadili au
ambavyo sitakiwi kuvifanya kilichonileta Mwanza ni kufanya show na
kufanya makubaliano na kusaini mkataba wa show yangu nyingine
itakayofanyika Dar es Salaam" alisema Nuh Mziwanda
No comments