MGANGA Abambwa Akimroga Mwanamuziki Darassa
Kufuatia uwepo wa madai kwamba wapo waganga wanaotumika kuwaroga
wasanii, hususan wale ambao nyota zao zipo juu, Kitengo Maalum cha
Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers kimeingia mzigoni na
kufanikiwa kumnasa sangoma mmoja maarufu ambaye aliingia kazini kuvuta
nyota ya mkali wa Hip Hop anayesumbua kwa sasa, Shariff Thabeet
‘Darassa’, twende pamoja!
TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini kilinyetisha kuwa, wengi wa waganga hao wapo maeneo ya Tandale, Mwananyamala na Bagamoyo, Pwani ambapo chanzo kiliahidi kutoa ushirikiano kwa mganga huyo ambaye kijiwe chake kipo maeneo ya Mwananyamala jijini hapa.
“Mbona wapo wengi tu, wakiona staa anatamba kama vile Diamond (Nasibu Abdul), Ali Kiba na wengineo, anawapokea hawa wasanii wadogowadogo wanaochipukia na kuwaambia atamshughulikia mmoja wa wasanii hao wanaowika na kudai anaichukua nyota yake kisha kumpa huyo mchanga,” kilisema chanzo hicho makini.
AJALI YA DARASSA YATAJWA
Kama hiyo haitoshi, chanzo hicho kiliweka wazi kuwa kutokana na wimbi la wasanii hao chipukizi kusaka nyota za wasanii wakubwa, watu wamekuwa wakiihusisha ajali ambayo Darassa ameipata hivi karibuni mkoani Shinyanga kwamba kuna mtu alikuwa anaisaka nyota yake.
“Yaani we acha tu, unaambiwa ile ajali nayo pia ilipangwa ili watu wampoteze, wachukue nyota,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupata madai hayo na kuyafanyia ‘upembuzi yakinifu’, haraka sana OFM iliingia mzigoni kwa kuanza kupanga mikakati ya kumuweka kwenye rada zake mganga huyo ambaye ni maarufu sana maeneo hayo.
SKRIPTI IKAPANGWA HIVI
OFM ilimchagua kamanda wake mmoja ambaye alijifanya ni msanii chipukizi wa Bongo Fleva hivyo anataka kutoka na kwamba anaihitaji nyota ya Darassa anayetarajia kuangusha shoo kali ya michano na mkali wa Hip Hop, Ibrahimu Mussa ‘R.O.M.A’ kwenye mkesha wa Mwaka Mpya ndani ya Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakheem jijini hapa.
Mipango yote ilipokamilika, ‘msanii’ huyo aliongozana na OFM wengine wawili waliojifanya ni watu wanaomsapoti kwenye kazi zake kwenda kwa sangoma huyo, baada ya kufika walimkuta akiwa ndani na baadaye aliwakaribisha kwenye chumba chake.
MANDHARI YA CHUMBA
Chumba hicho kilionekana si cha ‘mbavu za mbwa’, kama sangoma wengine wanavyotumia kuishi huko msituni, ni chumba cha kawaida na ndani yake kuna kitanda kikubwa pamoja na vioo kila kona na mazagazaga mengine vikiwemo vyombo na majani makavu na mabichi ambayo sangoma huyo alidai kuwa ni dawa za kienyeji.
Baada ya kukaribishwa msanii (OFM) alieleza shida yake kuwa alikuwa anataka kufanikiwa kimuziki na ikiwezekana achukue nyota ya Darassa, yule sangoma akamwambia asikonde, amefika na shida yake imeshakwisha.
“Yaani hapa ndiyo umefika, ondoa shaka hilo ni dogo sana kwangu,” alisikika mganga huyo.
AVUJISHA SIRI ZA WATEJA
Kuonesha kwamba yupo vizuri na amebobea kwenye fani hiyo, mganga huyo alizidisha mbwembwe za kujinadi hadi kujikuta akivujisha siri za wateja wake bila kujua.
“Yaani hapa mmefika, wenzenu kibao wamefika hapa na nimewasaidia…kina (anataja majina), wote hao wamefanikiwa kutokea hapa kwangu,” alijinasibu mganga huyo mbele ya vinasa sauti vya OFM.
AWAVUTA HADI WASINDIKIZAJI
Mganga noma, akaona asiishie kwa yule msanii pekee, alianza kutaja pia matatizo ya waliomsindikiza msanii huyo huku akiwaambia kama wote walikuwa wanataka kusaidiwa watoe kila mtu shilingi 10, 000.
WAMUOMBA WAKAJICHANGE
OFM hawakuwa na ubishi, walichofanya ilikuwa ni kumuomba sangoma waende wakamchukulie pesa hizo (lengo ni kujipanga vizuri kimbinu) na kumuahidi kuwa baada ya muda wangerejea.
WAREJEA
Baada ya nusu saa, OFM walirudi tena kwa sangoma na baada ya kufika walimwambia msanii peke yake ndiye afanyiwe matambiko ili afanikiwe kwenye mambo yake ya kimuziki na wale wengine, watafanyiwa siku nyingine.
SHUGHULI YAANZA
Yule sangoma alikubali na akamwambia OFM msanii akae kwenye kigoda kisha akampa kibuyu na kumwambia azungushie miguuni, kiunoni, kifuani na kichwani mara saba na baada ya hapo akaanza kumchanja chale kwa wembe (ni mpya, OFM ilihakiki kwanza) akimpaka dawa.
AMTABIRIA ‘MSANII’ MAZITO
Baada ya zoezi hilo, mganga alimhakikishia baada ya hapo ni lazima angekuwa juu kiasi cha kumfunika Darassa ikiwezekana kupiga kolabo mpaka za kimataifa na wakali wa Marekani kama akina Curtis Jackson ‘50 Cent’.
TUJIUNGE NA SANGOMA LIVE
Sangoma: Nyota yako nikiiangalia hapa naiona ipo juu sana! (alimwambia OFM huku akiendelea na zoezi la kumchanja chale.)
Msanii: Aisee….
Sangoma: Ndiyo hivyo! We umewahi kuwa karibu na Darassa?
Msanii: Ndiyo, kuna kipindi nilitaka kufanya naye ngoma (wimbo).
sangoma-akimroga-darassa-13Kamanda wa OFM akitekeleza masharti ya Sangoma.
Sangoma: Ni kweli masharifu wangu wananiambia, tena alichukua nyota yako, wewe ni msanii mkubwa sana, umefungwa usijiamini, tena hata ukiingia kwenye mambo ya kuigiza utafanya vizuri sana.
Msanii: Aisee nifanyie mambo niwike.
Sangoma: Usijali. Mimi ndiye Chief (anataja jina lake kamili) kijana wa Usambaani, kwangu mwisho wa reli, ndiyo maana sihitaji kuweka hata bango, kazi yangu inajitangaza yenyewe.
Ukweli ni kwamba sangoma huyo wakati wote alionekana akihenya sana akidai anaichukua nyota ya Darassa lakini alikuwa akizungumza mambo mengi juu ya msanii wa OFM maana hata kuwa karibu na Darassa, OFM huyo hajawahi.
MASHARIFU WAWATAKA NA WASINDIKIZAJI
Baada ya mganga huyo kupiga porojo nyingi, sangoma huyo aliwaambia pia jamaa wa karibu waliomsindikiza msanii huyo kuwa masharifu wake wamemwambia ni lazima nao wachanjwe pia dawa.
Hilo lilifanyika na baada ya hapo sangoma alimtaka yule aliyejitambulisha kama ni msanii kwenda kuoga dawa bafuni pamoja na ndugu zake, baada ya hapo akawaambia kuwa zoezi lililofuatia ni yeye kwenda kununua dawa zingine kwa ajili ya kwenda kuoga baharini kisha kuchinja kuku na tayari msanii wa OFM angekuwa amesafishwa na kumfunika Darassa.
OFM WAKABIDHI MTONYO
Baada ya hapo, OFM waliweka fedha kwenye chombo maalum cha huyo sangoma kisha kuondoka zao, huku mbele wakitafakari kwani maneno mengi aliyokuwa akiyazungumza mganga huyo hayakuwa na ukweli wowote.
DARASSA ANASEMAJE?
Amani lilimvutia waya Darassa na kumueleza kuhusu ishu hiyo ya mganga, alipopatikana hewani, alicheka na kupuuza.
“Hahaha! Huyo anajisumbua, namtegemea Mungu. Niwasihi mashabiki wangu wazidi kunisapoti na mkesha wa Mwaka Mpya waje pale Dar Live kushuhudia michano yangu na ya R.O.M.A,” alisema Darassa.
NENO LA MHARIRI
Ni vyema waganga wa namna hii wakajirekebisha na serikali ikiwezekana iingilie kati kwani wapo waganga wanaochukua pesa za watu wengi kwa kigezo cha kuwatafutia nyotaWATCH

No comments