MIMBA YA NISHA KUMBE ILIKUA NI KIKI TU
Kila mmoja ilimsikitisha story ambayo mwanadadaNisha alikuwa akitupanga na kutuaminisha kuwa amebakwa na aliyekuwa mpenzi wake na kupelekea kupata ujauzito.
Kitu ambacho kilizua utata mkubwa sana na maswali ya sintofahamu na kupelekea wasanii ambao wamewahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Nisha kuingizwa katika sakata hilo akiwemo Nay wa Mitego.
Siku chache zilizopita Nisha alisikika katika vyombo vya habari akifunguka ukweli kuhusu ujauzito wake na kudai kuwa ni kazi ndiyo ilimfanya kudanganya hivyo lakini yeye sio mjamzito. Kitu ambacho kiliwatoa mapovu wengi ambao walikuwa wakimfuatilia mwanadada huyo.
Soudy Brown amepiga story na mwanadada huyo kwenye U-Heard ya leo December 22 na amefunguka mengi kuhusu kitendo chake hicho cha kudanganya umma. Soudy pia alimvutia waya Nay wa Mitego ili kutaka kujua ana kipi cha kuzungumza baada ya story hizo za mwanadada Nisha.
No comments