Header Ads

PAUL Makonda Amtaka DC wa Ubungo Kufuata Nyayo zake

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo (Alhamisi) amemwapisha Mkuu mpya wa Wilaya ya Ubungo, Kisale Makori na kumtaka kutokaa ofisini na kusubiri taarifa  badala yake atoke nje na kusikiliza kero za wananchi wa wilaya hiyo.

Makonda amesema changamoto kubwa ya watendaji ni uwajibaki na kwamba baadhi yao hupenda kusubiri kupelekewa taarifa za wananchi ofisini badala ya kuwafuata wananchi katika maeneo yao.

"Naomba Makori usiwe mtu wa kusubiri taarifa ofisini pekee.Wanaubungo  wanamatumaini  makubwa na wewe kwa sababu umeaminiwa na Rais (John Magufuli),"amesema Makonda.

No comments

Powered by Blogger.