Header Ads

FEROOZ " Inaniwia Vigumu Kuacha Madawa ya Kulevya"


Msanii mkongwe wa muziki Ferooz Mrisho ambaye katika miaka ya 2000 alitamba na wimbo wa Starehe ambaye kwa sasa ameathirika na dawa na matumizi ya Madawa ya kulevya, amedai inamuwia vigumu kuachana na matumizi ya dawa hizo. Muimbaji huyo amedai amejikuta akitenga bajeti kubwa ya fedha kwa matumizi ya kutumia dawa.

“Ninawaomba wasanii wenzangu wasitumie dawa maana ni vigumu kuacha. Natamani sana kurudi kama zamani ili heshima yangu iwepo ila inanisumbua, lakini naamini iko siku,” Ferooz aliliambia gazeti la Mtanzania. Hata hivyo muimbaji huyo alipoulizwa ni wapi anaponunua Madawa hayo hakuwa tayari kutaja.

No comments

Powered by Blogger.