Header Ads

Yaya Toure asema hapangi kuhama Manchester City

Yaya Toure amesema hatatafuta klabu ya kuhamia kipindi cha kuhama kwa wachezaji mwezi Januari na badala yake ataangazia kusaidia klabu yake ya Manchester City.
Toure, 33, anahudumu miezi sita ya mwisho ya mkataba wake Etihad na yuko huru kuanza kuwasiliana na klabu nyingine.

Lakini amesema: "Kwa sasa naangazia City. Siku za usoni zipo lakini kwa sasa ligi bado haijamalizika."
Raia huyo wa Ivory Coast alirejeshwa kucheza Novemba baada ya kuwekwa kwenye baridi kwa miezi mitatu kutokana na matamshi ya wakala wake.
Meneja wa City Pep Guardiola alikuwa ameapa kutomchezesha Toure hadi wakala wake Dimitri Seluk aombe msamaha kwa kusema Toure aliaibishwa kwa kutojumuishwa kikosi cha City kinachocheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Toure aliomba msamaha kwa niaba ya Seluk mwezi Novemba na amekuwa kiungo muhimu katika timu yake.

Aliwafungia mabao mawili ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Crystal Palace tarehe 19 Novemba.

BBC SWAHILI

No comments

Powered by Blogger.