CCM yamjibu hivi Mjane wa Kapteni Komba kuhusu mafao ya mumewe
Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kimemtaka Mjane wa Marehemu, Kapteni Komba, Bi.
Salome Komba kufuatilia malipo ya mafao ya mumewe kwa uongozi wa kundi
la Tanzania One Theatre (TOT) ambako ndiko alikokuwa akifanyia kazi.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rodrick Mpogolo, ametoa maelekezo hayo ikiwa
ni siku moja tu baada ya Salome kukaririwa akimuomba Mwenyekiti wa
CCM, Rais John Magufuli aingilie kati kumsaidia ili alipwe mafao ya
marehemu mume wake yanayofikia Shilingi Milioni 75.
Mpogolo
amesema ofisi yao haiwezi kulizungumzia suala hilo kwa sababu masuala
yanayohusu fedha yanapaswa kufafanuliwa vyema na uongozi wa kundi lao la
TOT ambako Komba alikuwa akifanya kazi.
“Ofisi
yao haiwezi kulizungumzia kwa sababu masuala yanayohusu fedha yanapaswa
kufafanuliwa vyema na uongozi wa kundi lao la TOT ambako Komba alikuwa
akifanya kazi,” amesema.
Kwa
mujibu wa Bi. Salome, hadi sasa wakati mumewe akitimiza miaka miwili
tangu afariki dunia, CCM imemlipa Shilingi Milioni 4.5 tu ikiwa ni
sehemu ya malipo hayo huku akifuatilia kwa muda mrefu bila mafanikio
kupata kiasi kilichobaki cha Shilingi milioni 70.5 bila mafanikio.
Komba
aliyezaliwa mwaka 1954, alifariki dunia Februari 28, 2015 na kuzikwa
Mkoani Ruvuma ambako enzi za uhai wake alijizolea umaarufu mkubwa
kutokana na umahiri wake katika kutunga na kuimba nyimbo mbalimbali za
kwaya, hasa za kukipigia debe chama chake (CCM) wakati wa kampeni
mbalimbali za uchaguzi.
No comments