Seven Mosha: Kuna wakati mashabiki wa Alikiba wanatunyima usingizi
Meneja wa Alikiba, Seven Mosha amekiri kuwa pressure wanayoipata kutoka kwa mashabiki wa staa huyo ni kubwa na wakati mwingine huwakosesha usingizi.
Seven ameiambia Bongo5 kuwa pindi kazi za Ali zinapochelewa kidogo kutoka, hukuiona cha mtema kuni kutokana na shinikizo toka kwa mashabiki wake.
“Ukiwa na kipaji kama hicho, na potential hivyo, sio rahisi watu waelewe vitu kibiashara,” amesema. “Na saa zingine vile vile unaweza kuvuka kibiashara ukaspeed up issue zaidi. Kwahiyo Alikiba amekuwa msanii ambaye amekuwa highlighted na upande wa Sony kwamba speed up the situation,” ameongeza.
Seven anasema pressure kubwa huipata pindi mashabiki wa Alikiba wakikasirika. “When they are not happy, we all are not happy,” anasema.
Nilipomuuliza kama mashabiki wanawanyima usingizi, Seven amesema, ” Oh Yeah, kabisa, na politics ukichanganya huko ndani basi vurugu.”
Meneja huyo amekiri kuwa wakati mwingine licha ya kupost vitu Instagram huacha kusoma comments sababu zinaweza kumtoa kwenye reli.
No comments